Kuhusu UWASE
Katiba ya UWASE inaeleza kuwa umoja umejengwa katika misingi ya uhuru, undugu, amani, usawa na demokrasia. Makao makuu yako Mkoa wa Mara, Kijiji cha Seka; anuani ni S.L.P 717, Musoma Mara.
Madhumuni
- Kuongeza mshikamano na undugu bila ubaguzi wa rangi, dini au kabila.
- Kushirikiana, kusaidiana na kufarijiana katika shida na faraja.
- Kubuni na kutekeleza miradi ya kiuchumi na maendeleo.
- Kujitolea katika maendeleo ya Kijiji cha Seka.
- Kuwa mfano wa ushirikiano kwa jamii.
UWASE ni jumuiya ya kiraia isiyofungamana na siasa za ndani au kimataifa.